SIMU ZA MKONONI NI MATATIZO KATIKA MAHUSIANO?

Monday, June 42comments



Habari wapendwa karibu mara nyingine tena katika blog yako hii uipendayo tuzungumze mambo yanayotuzunguka katika maisha halisi tunayoishi (Duniani) endelea….
Leo napenda tujadiliane suala la simu za mkononi. Suala hili bilashaka limeshazungumzwa mara nyingi sana katika vyombo mbali mbali vya habari, simu za mkononizina faida nyigi tu ila wahenga walisema “kila lenye faida halikosi hasara”, lakini mimi napenda kuingia ndani zaidi na kulihusisha na suala la mahusiana kati ya wapendanao.
Unawezaje kuyafanya  mahusiano yako yadumu na yasivunjike kwa sababu tuu ya simu yako au ya mwenza wako?
Watu wengi sana wamekuwa wakijikuta katika wakati mgumu kwa sababu ya kitu hiki kidogo, simu!!! Hebu jiulize! “kwanini wewe unamiliki simu yako na ya mpenzi wako? kwanini humuamini? kwanini nawe pia hujiamini?  Je kama anakupenda kwa dhati anaweza kukudanganya? kwa nini usimpe nafasi ajitambue kuliko kuwa mlinzi wa simu yake? Unahisi wewe ukijua anawasiliana na nani kutwa nzima ndo utakuwa na furaha maishani au utaongeza matatizo moyoni mwako na katika mahusiano yenu?
Maswali hayo machache tujiulize kabla hatujaenda mbali. WHY? KWANINI?
Katika hali ya kawaida tu ukikagua simu ya mweza wako kila wakati utajikuta badala ya kupata faraja moyoni unajikuta unapata stress ambazo hazina mpango!! Unaumiza moyo wako maana utajikuta unagundua vitu vingi vya ajabu na mahusiano yanaanza kuvurugika!

                                                        
                                                             JE! NI NINI SULUHISHO?

Uaminifu ni kitu kizuri, muonyeshe kuwa unamuamini sana. usimfuatilie kupita kiasi hasa katika simu yake ya mkononi. Mwache awe na uhuru na simu yake, muonyeshe kuwa bila yeye unaweza kuishi maana ukifuatilia sana simu yake, utaumia na atabaini kuwa bila yeye hujiwezi sikio wala ndewe!!
Unajua mtu ukimpa uhuru sana hata yeye anajishtukia na kushangaa inakuwaje, kwa hiyo hata kama anafanya ujinga atajirudi kwa kuona ni kiasi gani anakukosea na wakati wewe umetulia na unampenda.
Mpende kwa dhati, lakini haimaanishi ndo uwe mlinzi wa simu yake ya mkononi, utajiumiza bure na mapenzi wala hutoona raha yake. Tulia, anayekupenda utamjua tu wala hana macho juu, hana mawasiliano yasiyokuwa na maana, anatulia na wewe.

KUDONDOSHA COMMENT YAKO.
Share this article:

+ comments + 2 comments

June 4, 2012 at 5:05 PM

Lakini wakati mwengine kuwa na simu kupelekea kuwa na mawasiliano na m2 mwengine hata muda mbaya, mfano Ucku, mda mmekaa pamoja. so kuna mda simu ni tatizo!!!!

Anonymous
June 10, 2012 at 1:42 AM

i like

Post a Comment

Unaonaje huu Muonekano?

 
Support : Management

Copyright © 2011. Al-amini Official blog - All Rights Reserved
Template Modify by Al-Amini
Proudly powered by Blogger