Tabia Kumi (10) Za Msichana Anaye Kupenda Lakini Anashindwa kukwambia

Wednesday, April 10 comments





Ukiachana na mada ambazo ulishazisoma katika blog hii kuhusu pande zote mbili yaani kwa mwanaume na mwanamke, naomba leo ufahamu hizi tabia kumi (10) za msichana anayekupenda lakini anashindwa kuelezea hisia zake kwako.
 
1. Atakutega kupata attention yako. Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama unampenda au lah! Mfano wa mambo hayo ni kujifanya anaumwa na kuangalia respond yako kwake ni kiasi gani unamjali na kiasi gani utahangaika kwa ajili yake au laa.

2. Haoni aibu kugusa sehemu yako ya mwili. Msichana anayependa haoni aibu kukushika mkono ama kukutomosa au hata kukumbatia. Kwa kufanya hivyo hujua kuwa kwa asilimia kubwa hisia za kushikana kwenu kutamrahisishia kazi ya kuwa na wewe


3. Kucheka kwa nguvu hata kwa kitu kisicho chekesha endapo wewe umezungumza. Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli

4. Wivu.
Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unachart nao na ukiwaita majina ya kimahaba. Hapendi.

5. Anakumbuka siku zako muhimu. Hukumbuka kama vile siku yako ya kuzaliwa hatoweza kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifaulu mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza


6. Eye contact anapenda kukuangalia machoni muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utaelewa ni kiasi gani anakupenda kupitia vile ambavyo anakuangalia.
Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda si wote wana ujasiri wa kuwatazama wapenzi wao.

7. Hupenda kukaa mda mwingi na wewe. Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya ili ajumuike na wewe.

8. Yupo tayari kuangamiza. Kama msichana anakupenda yupo tayari kusacrifice. Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye anaweza akafanya kwa mtu mwingine. Utaona vipi huyo msichana alivyo kwako na wa wengine. Yaani yupo tayari yeye akose lakini wewe upate na kwa mwingine anaweza akamwambia hana alichoombwa lakini akakupa wewe kama pesa na vitu vingine.
 
9. Anachukulia matatizo yako kama ni yake. Unapomueleza kuwa ana tatizo anajali tatizo lako kama vile ni lake na hujisikia vibaya sana na kuhuzunika na atafanya lolote ili aweze kukusaidia utoke katika hilo tatizo.


10. Mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakuambia anakupenda. Kwa kuwa anakupenda endapo ikatokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose.

Mwanaume wewe bado hujajua kama Unapendwa tu AU?.
Share this article:

Unaonaje huu Muonekano?

 
Support : Management

Copyright © 2011. Al-amini Official blog - All Rights Reserved
Template Modify by Al-Amini
Proudly powered by Blogger