Utafiti umeonesha kuwa, katika kila wanawake kumi wanaokwenda kazini asubuhi, saba wanaporudi nyumbani jioni huwa wemebeba mifuko yenye vitu kama chakula, “viguo” na zawadi nyenginezo kwa ajili ya watoto na wapenziwao.
Utafiti wa kina uliofanya na Meza yetu hii umebaini kuwa kati ya jinsia mbili zilizopo duniani, wanawake ndiyo wanaongoza kwa kukumbuka familia na kuamua kuwabebea chochote kuliko wanaume.
Wakati Utafiti kwa wanawake umeona hilo, wanaume wao, katika kila kumi wanaokwenda kazini asubuhi, watatu tu ndiyo wanweza kukumbuka kubeba chochote kwa ajili ya familia.
Saba waliobaki, mara nyingi hushindwa kubeba chochote kwa
sababu baada ya kutoka kazini huanzia Baa kabla ya kurejea nyumbani na wakiwa
baa vitu wanavyonunua ni vile vinavyowahusu, na wakirudi nyumbani labda wamenunua vitu kwa ajili yao binafsi kama viatu, mashati, tai n.k
TOA MAONI YAKO JUU YA HILI