Ni suali moja ambalo halina majawabu ya moja kwa moja, lazima tuangalie vigezo zaidi kuliko kwa mtazamo wa kawaida. kama wewe unayo majibu usisite kutuandikia.
Mwanaume
anamuhitaji mwanamke zaidi kama msaidizi wake kuliko mwanamke
anavyomhitaji mwanaume na sema hivyo sio kwa kuegemea swala la ngono
bali kwenye maswala mengine mengi ya kimaisha.
Inasemekana kwamba wanawake ambao hawajaolewa wanaishi zaidi
ukilinganisha na wale walio ndani ya ndoa na Wanaume waliondani ya ndoa
huishi maisha marefu zaidi kuliko wale walio nje ya ndoa, umewahi
kujiuliza kwanini wataalamu wanadai hivo?
Tunapoanza kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na baadae maisha ya
ndoa (milele pamoja) tunakuja kuhisi kuwa hatuwezi kuishi bila wenza
wetu sio kwa vile wanatulisha na kutuvisha bali tunawapenda na pengine
ni kwa vile umri umeenda na unahofia kuwa "nani atanitaka na mikunjo
hii".
Mwanaume ni mwindaji na uwindaji huo sio wa kupata kitoweo tu (pesa)
bali kukupata wewe mwanamke pia, inasemekana kuwa wanaume wengi wanaamua
kuwa “single” au wagumu ku-commit karne hii kwa vile wanawake
hawawindiki tena.
Kwamba wanawake wamekuwa rahisi kupatikana (kukubali kirahisi) na hivyo
wanaume hawahisi kama unawafaa kama wapenzi wao wa kudumu kwa vile
hawakukuwinda bali ulijitega mwenyewe (kutokana na U-feminist a.k.a
Ubeijing wa wanawake wengi wakidhani ni Usawa).
Hali hiyo inasababisha wanawake wengi kukata tamaa na wanaume ambao
hawa-commit kwenye mahusiano ya kudumu.
YOUR COMMENTS PLEASE